Mnyama kupaa Afrika Kusini Septemba 24

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 Sep 2026
Mnyama kupaa Afrika Kusini Septemba 24

Klabu ya Simba imethibitisha kuwa Septemba 24 kikosi kitasafiri Afrika Kusini kuweka kambi ya maandalizi ya mechi za ligi kuu na michuano ya ligi ya mabingwa (CAFCL).

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ali amesema uongozi umewapa mapumziko wachezaji ambao hawana majukumu ya timu ya Taifa na watarejea Septemba 24 na moja kwa moja kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya kambi.

"Kambi hii imesimamiwa moja kwa moja na Rais wa heshima Mohamed Dewji 'Mo' ambaye ameona siku hizi 10 badala ya kuendelea kufanya mazoezi Bunju, timu iweka kambi ya muda mfupi Afrika Kusini kwa ajili ya utulivu na kufanya maandalizi yetu"

"Mwezi wa 10 utakuwa wa 'moto' kutokana na ratiba ya michuano mbalimbali ambayo Simba inashiriki hivyo kambi hii imezingatia mahitaji yetu kuelekea ratiba hiyo ngumu," alisema Ahmed

Ahmed amesema kambi hiyo haitawahusu wachezaji walioitwa kwenye majukumu ya timu za Taifa ambapo wachezaji 7 wameitwa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' ambao ni Nathaniel Chilambo, Vedastus Masinde, Bakari Msimu, Nickson Kibabage (majeruhi), Anthony Mligo, Yusuph Kagoma na Moricce Abraham

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
1h ago
READ MORE β†’
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
5h ago
READ MORE β†’
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
19h ago
READ MORE β†’
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
23h ago
READ MORE β†’
Huyu Libasse ni moto kweli
Huyu Libasse ni moto kweli
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
2d ago
READ MORE β†’