Mbao FC yarudi kileleni Ligi Kuu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
31 Aug 2018
Mbao FC yarudi kileleni Ligi Kuu
Mbao FC inaonekana kuimarika msimu huu baada ya leo kulazimisha suluhu ya bila kufungana dhidi ya Singida United kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara raundi ya tatu uliopigwa dimba la Namfua, Singida.

Mbao FC iko kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama saba, ikiwa imeshinda michezo miwili na kutoka sare mchezo mmoja.

Ligi hiyo itaendelea kesho Jumamosi, Septemba mosi kwa michezo mitano kupigwa kama inavyoonekana hapa chini;

Stand United vs Bishara
Coastal Union vs KMC
Mtibwa Sugar vs Mbeya City
Kagera Sugar vs African Lyon
Prisons vs Alliance

Baada ya michezo ya wikiendi hii, ligi itasimama kwa muda wa wiki mbili kupisha michezo ya Kimataifa kwa mujibu wa kalenda ya FIFA.

Simba iliyokuwa icheze na Lipuli FC kesho mchezo huo uliahirishwa baada ya wachezaji saba wa Simba kuitwa timu ya Taifa.

Hata hivyo kocha Mkuu wa Stars Emmanuel Amunike aliwaondoa wachezaji sita wa Simba isipokuwa Aishi Manula sababu ikielezwa kuchelewa kuripoti kambini.

Mapema leo Amunike alifanya mazungumzo na wachezaji hao na kuwahakikishia kuwa atawajumuisha kwenye kikosi cha Stars siku zijazo kama wataendeleza viwango vyao.

Amesema kwa sasa hatawatumia kwa kuwa tayari ameshaita wachezaji wengine kuchukua nafasi zao baada ya sintofahamu iliyojitokeza.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’