Yanga inaweza kusajili mchezaji mmoja kwa ajili ya hatua ya makundi CAF CC

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Apr 2018
Yanga inaweza kusajili mchezaji mmoja kwa ajili ya hatua ya makundi CAF CC
Droo ya Makundi ya kombe la Shirikisho Barani Afrika itafanyika kesho Jumamosi April 21 2018 jijini Cairo nchini Misri.

Michezo ya kwanza ya makundi inatarajiwa kufanyika katikati ya mwezi May 2018.

Kulingana na kanuni za CAF, Yanga inaweza kusajili hadi wachezaji saba kuwatumia hatua ya makundi ikitegemea idadi ya wachezaji iliyotuma mwanzo kikomo kikiwa wachezaji 30.

Hata hivyo Yanga ilituma majina ya wachezaji 29 mwezi Januari hivyo inaruhusiwa kuongeza mchezaji mmoja wakati huu wiki mbili kabla ya kuanza kwa hatua ya makundi.

Hata hivyo sheria zinawabana kuwa ni lazima mchezaji huyo asiwe ameshiriki michuano hiyo mwaka huu.

Hivyo hata kama Yanga itamsajili Djako Arafat wa Wolaitta Dicha, haiwezi kumtumia kwenye michuano hii mwaka huu.

Lakini pia pamoja na kusajili mchezaji mmoja, Yanga inaweza kukamilisha hatua iliyobaki kupata vibali vya beki Fiston Kayembe Kanku ambaye jina lake lilitumwa CAF mwezi Januari
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’