Straika wa Simba, Marcel Kaheza bado hajaanza kuaminiwa katika kikosi cha kwanza cha kocha wa timu hiyo Mbeligiji Patrick Asseums, jambo linalomuumiza kichwa na kufanya azidishe mazoezi ili siku akipewa nafasi afanye kweli.
Kaheza amesema kwamba kuna ushindani mkubwa wa namba katika safu ya ushambuliaji na kwamba waliobahatika kupewa nafasi wanafanya vyema, jambo linalomfanya kocha Asseums aendelee kuwaamini, huku yeye akisota.
"Napigania nafasi ambayo itafanya nionyeshe kile nilichonacho, hilo ndilo linanifanya nijitume kama vile naanza katika kikosi cha kwanza, ligi bado ndefu naamini ipo siku mashabiki watanielewa tu kwamba sijaja kutembea bali nipo kwa ajili ya kazi ndani ya kikosi cha Simba," alisema.
Alipoulizwa kwa ufinyu wa nafasi ya kucheza je anaweza akatetea rekodi yake ya mabao 14 aliyoyafunga msimu uliopita akiwa na Majimaji iliyoshuka daraja! Alijibu " Nikibahatika kupata nafasi ya kucheza ndoto zangu zitaanzia hapo, kwa sasa ngumu kujua nataka kufanya kitu gani nikiwa benchi," alisema.
Keheza alisema anaendelea kuwasoma wale ambao kocha anajaribu kuwapa nafasi mara kwa mara ambao ni Adam Salamba na Rashid Mohamed 'Mo' kwa kuwachanganya na wazoefu John Bocco na Meddie Kagere, wana vitu gani kisha anaenda kujiongeza na mazoezi.
"Mchezaji mzuri ni yule ambaye anajua ubora na mapungufu yake, ndio maana naangalia wenzangu wana vitu gani vya ziada ambavyo kocha anavipenda kwao kisha naenda kuvifanyia kazi katika mazoezi yangu binafsi," alisema.
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE