Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka kesho Jumamosi mchana kuelekea mkoani Mbeya kwa usafiri wa Ndege tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Mbeya City.
Yanga imetua kutoka Ethiopia usiku wa kuamkia leo.
Mchezo dhidi ya Mbeya City utapigwa kwenye dimba la Sokoine keshokutwa Jumapili, April 22 2018.
Kocha Mkuu wa Yanga Noel Mwandila amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo huo baada ya kazi ngumu ya kufuzu makundi kombe la Shirikisho.
Yanga itasafiri kwenda Mbeya bila kiungo wake Papi Kabamba Tshishimbi aliyeumia kwenye mchezo dhidi ya Wolaitta Dicha.
Kulingana na Daktari wa Yanga, Dk Edward Bavu, Tshishimbi atabaki jijini Dar es salaam kwa uchunguzi zaidi wa maumivu aliyopata kwenye mguu wake wa kulia.
Hata hivyo habari njema ni kurejea kikosini kwa Ibrahim Ajib na Andrew Vicent ambao hawakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kilichosafiri nchini Ethiopia.

ADVERTISE HERE