Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba wameendeleza rekodi nzuri ya ushindi katika kampeni ya kutetea ubingwa wake baada ya kuilaza Mbeya City mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa.
Huo ni ushindi wa pili kwa Simba na imefanikiwa kutunza rekodi ya ushindi kwa asilimia 100.
Simba iliyotawala mchezo huo tangu dakika ya kwanza, ilijipatia mabao yake kupitia kwa mshambuliaji wake hatari Meddie Kagere ambaye mpaka sasa ndiye aliyefunga mabao yote ya Simba.

Mabao yake ya leo aliyafunga kwa kichwa ambapo bao la kwanza alifunga kwenye dakika ya 11 akiunganisha krosi ya Shiza Kichuya huku la pili akilifunga kwenye dakika ya 45 akiunganisha krosi ya Asante Kwasi.

Kagere amefikisha mabao matatu na mapema tu anaongoza orodha ya wapachika mabao katika ligi ambayo sasa iko mzunguuko wa pili.
Katika mchezo mwingine uliopigwa mapema, African Lyon ililazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Alliance.

ADVERTISE HERE