Okwi awashukuru mashabiki kwa kujitokeza kwa wingi CCM Kirumba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 Aug 2018
Okwi awashukuru mashabiki kwa kujitokeza kwa wingi CCM Kirumba
Mshambuliaji kinara wa mabao katika kikosi cha Simba Mganda Emanuel Okwi amewashukuru mashabiki wa timu hiyo waliojitokeza kwa wingi kwenye dimba la CCM Kirumba na kuisaidia Simba kutwaa Ngao ya Jamii kwa kuichapa Mtibwa Sugar mabao 2-1.

Okwi aliyeshindwa kumaliza dakika 90 za mchezo huo baada ya kupata majeruhi, amesema ushirikiano wa mashabiki, benchi la ufundi na wachezaji ndio uliofanikisha wao kuibuka washindi wa Ngao ya Jamii kwa msimu wa pili mfululizo.

"Nachukua nafasi hii kuwashukuru wachezaji wote, benchi la ufundi, viongozi na mashabiki wote wa Simba Sports Club kwa umoja tulionyesha jana na kufanikiwa kushinda Ngao ya Jamii. Mapambano yanaendelea. Mkubwa Mungu," amesema Okwi.

Mabao ya Simba kwenye mchezo wa jana yalifungwa na Meddie Kagere na Hassani Dilunga huku bao la kufutia machozi kwa upande wa Mtibwa Sugar lilifungwa na Kelvin Sabato Kiduku.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
11h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
14h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’