Tasnia ya Sanaa nchini Tanzania imepata pigo kwa kuondokewa na mchekeshaji maarufu zaidi nchini Amri Athumani 'King Majuto'.
Mzee Majuto amefariki jioni ya leo akiwa anapatiwa matibabu Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa.
Alirejea hivi karibuni kutoka nchini India alikokwenda kupatiwa matibabu zaidi ya maradhi yaliyokuwa yanamsumbua.
Lakini Mwenye ez Mungu amempenda zaidi.
Mzee Majuto alizaliwa mwaka 1948 jijini Tanga na kusoma shule ya Msambwini jijini humo.
Alianza kuigiza mwaka 1958 akiwa na umri wa miaka 9 akiigiza katika majukwaa.
Licha ya kuigiza, Mzee Majuto alikuwa mtunzi na mwandishi mzuri wa miswada ya filamu za kuchekesha na hata za maudhui tofauti.
Alikuwa muigizaji wa kwanza kuandaa kazi zake katika mikanda na kuuza akiwa na Tanzania Film Company ( TFC)
Mungu ailaze roho yake mahali pema, peponi AMEN.

ADVERTISE HERE