Welayta Dicha wanafungika muhimu kujipanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Apr 2018
Welayta Dicha wanafungika muhimu kujipanga
Kikosi cha Yanga kitashuka kwenye uwanja wa Taifa siku ya Jumamosi, April 07 kuc heza mchezo wa kwanza wa mtoano kusaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Yanga ina dakika 180 za kufanya kile ilichofanya miaka miwili iliyopita, kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Yanga inayo nafasi kubwa ya kutinga makundi itakapoivaa Welayta Dicha, mabingwa wa kombe la FA la Ethiopia.

Muhimu ni kuhakikisha hairudii makosa kwa kutumia vyema uwanja wa nyumbani.

Moja ya sababu zilizopelekea Yanga kuondoshwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa ni kupoteza mchezo wa kwanza uwanja wa Taifa dhidi ya Township Rollers.

Yanga haikufungwa ugenini kama ingepata ushindi nyumbani ingetinga hatua ya makundi.

Welayta Dicha sio timu yenye jina kwenye soka la Afrika. Kama ilivyokuwa kwa Township Rollers sio miongoni mwa timu za kuogopwa kabisa.

Kwenye msimamo wa ligi kuu ya Ethiopia inashika nafasi ya nane. Ikiwa imeshinda michezo sita na kupoteza michezo sita huku ikitoka sare kwenye michezo mitano.

Haina safu kali ya ushambuliaji kwani kwenye ligi katika michezo 17 imepachika mabao 15 tu na kuruhusu mabao 14.

Ni timu ambayo haitengenezi nafasi nyingi za kufunga lakini inatumia vyema nafasi chache inazopata.

Ikitangulia kufunga ina kawaida ya kujilinda zaidi na sio kutafuta mabao mengi. Ndio maana michezo mingi imekuwa ikishinda kwa bao moja au mawili.

Hivyo njia rahisi ya kupata ushindi dhidi yao ni kutangulia kuwafunga.

Welayta imefika hatua ya mtoano ya michuano ya kombe la Shirikisho kwa kuziondoa Zimamoto ya Zanzibar na Zamalek ya Misri.

Ilipokwenda kucheza Zanzibar kwenye mchezo wa hatua ya awali, ililazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Zimamoto kabla haijakwenda kushinda nyumbani kwa bao 1-0.

Mchezo dhidi ya Zamalek ilishinda 2-1 nyumbani na pia ikafungwa 2-1 nchini Misri na ikafanikiwa kupenya kupitia changamoto ya mikwaju ya penati.

Ushindi wa aina yoyote nyumbani utaiweka Yanga kwenye mazingira mazuri ya kutinga hatua ya makundi.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’