Poulsen atangaza kikosi cha Stars U-23

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
3 Nov 2017
Poulsen atangaza kikosi cha Stars U-23
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Vijana Kim Poulsen leo ametangaza majina ya wachezaji wanaounda kikosi cha timu ya Taifa chini ya umri wa miaka 23.

Timu hiyo imeundwa maalumu kwa ajili ya kushiriki michuano ya Olympiki ambayo fainali zake zitafanyika nchini Japani mwaka 2020.

Wachezaji waliochaguliwa ni wale wenye umri wa kuanzia miaka 20 kushuka chini.

Timu zilizotoa wachezaji wengi katika kikosi hicho ni Azam wachezaji watano, Simba (1), Yanga (4), Mbeya City (3), Majimaji (2), Singida United (2), Stand United (2) na Mwadui (2).

Timu nyingine zilitoa wachezaji wanaounda kikosi hicho ni Ruvu Shooting, Prisons, Miembeni City, Njombe Mji, JKU, Mwadui, Mtibwa, Ndanda na Ashanti United.

Kocha msaidizi wa Ngorongoro Heroes, Oscar Milambo alisema wameita kikosi hicho wakiwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri.

"Benchi la ufundi tumejiridhisha kiwango cha hawa wachezaji baada ya kuwafuatilia kwa ukaribu katika timu zao ambazo idadi kubwa zipo Ligi Kuu.

"Mkakati wetu ni kuhakikisha tunafanya vizuri katika mechi zilizo mbele ya kuwania kushiriki mashindano ya Olimpiki yatakayofanyika Tokyo, Japan 2020.

Wachezaji walioitwa ni: Metacha Mnata, Joseph Prosper, Masoud Abdallah, Abbas Kapombe na Yahya Yahya Zayd (Azam FC), Cleotas Sospeter, Yusuph Mhilu, Emmanuel Martin na Geoffrey Mwashiuya (Yanga), Ismail Aidan, Salum Kihimbwa na Hassan Mganga (Mtibwa) na Eliud Ambokile, Emmanuel Kakuti na Medson Mwakatundu (Mbeya City).

Wengine ni Liza Mafwea na Bakari Kijuji (Prisons), Adam Salamba na Stanley Angeso (Stand United), Award Salum na Agaton Mapunda (Njombe Mji), Omary Mponda, Ayoub Masoud na Baraka Majogoro (Ndanda FC), Salum Chuku na Yusuph Kagoma (Singida United), Derushi Shaliboko (Ashanti United), Awesu Ally (Mwadui), Mohammed Jailan (Miembeni City), Yusuph Mlipili (Simba), Faisal Salum (JKU), Joseph Ilunda (JKT Ruvu), Idrissa Mohammed (Majimaji) na William John (Ruvu Shooting).
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
3h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
9h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
12h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’