Anaitwa Papi Kabamba Tshishimbi

Yanga Damu By Yanga Damu
β€’
24 Jul 2017
Anaitwa Papi Kabamba Tshishimbi
Ukweli ni kwamba Yanga haijaanza kumfuatilia kiungo huyu makabaji leo. Taarifa zake zimepamba moto siku chache hizi baada ya kutua Dar kwa siri kufanya mazungumzo na uongozi wa Yanga.

Yanga imekuwa na dhamira ya dhati ya kupata kiungo mkabaji mwenye uwezo wa hali ya juu baada ya Justine Zulu 'Mkata Umeme' kuchemsha kwenye nafasi hiyo.

Sasa huyu kiungo Papi Kabamba Tshishimbi anachezea Mbabane Swallows na alikuja Tanzania kwa mara ya kwanza akiwa na kikosi cha timu hiyo kucheza na Azam kwenye mchezo wa kwanza wa mtoano kombe la shirikisho.


Papi Kabamba Tshishimbi

Baada ya kiwango alichoonyesha kumvutia kocha George Lwandamina, mara moja aliagiza mchezaji huyo afuatiliwe kwa ukaribu zaidi.

Hivyo alianza kufuatiliwa hapo na hata kocha Lwandamina kabla hajatua Dar kutoka likizo Zambia alipitia Swaziland kutizama moja ya michezo ya Mbabane kujiridhisha na ubora wa kiungo huyo.

Tshishimbi anaweza kuwa tiba sahihi ya ugonjwa wa kiungo mkabaji kwa Yanga. Huyu jamaa ana uwezo mkubwa sana wa kukaba pia ni mzuri sana kwenye kupeleka mashambulizi mbele.

Hapotezi mipira kizembe na pasi zake nyingi zina macho.

Ana uwezo mkubwa sana wa kupiga pasi ndefu. Kwa wale waliomshuhudia Athumani Iddi 'Chuji' wakati huo akiwa kwenye kiwango cha juu Yanga, huwezi kumtofautisha sana na huyu jamaa katika utaalamu wa kupiga pasi ndefu.


Papi Kabamba Tshishimbi akitimiza majukumu yake dimbani

Kuwa na mchezaji kama huyu kikosini ni faida kubwa hasa ukiangalia aina ya washambuliaji waliopo Yanga sasa.

Sasa tusubiri habari njema kutoka kwa uongozi kuhusu huyu jamaa kwani upo uwezekano mkubwa akamwaga wino Jangwani baada ya mazungumzo kukamilika.

Ikumbukwe Yanga ina nafasi mbili za wachezaji wa Kimataifa hivyo iko makini sana katika kujaza nafasi hizo na ndio maana baadhi ya wachezaji bado wanafanyiwa majaribio.

Wachezaji wa Kimataifa ambao wamesajiliwa ni Youthe Rostand, Amissi Tambwe, Donald Ngoma, Obrey Chirwa na Thaban Kamusoko.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na mmoja wa wajumbe wa Kamati ya usajili, Yanga inakusudia kujaza nafasi zote mbili kwa kusajili kiungo mkabaji na beki kiraka.

Ujio wa Kabamba sasa umemfanya kiungo Mkameruni Fernando Bongyang kuingia vitani na Mnigeria Henry Tony Okoh kuwania nafasi moja iliyosalia.

Bongyang atawania nafasi hiyo na Mnigeria huyo ili kuziba nafasi ya beki wa kati, kutokana na uwezo aliokuwa nao wa kucheza pia nafasi hiyo muhimu.

Wawili hao waliokuwa wakijifua kwenye mazoezi ya gym, wataanza kuonyeshana kazi kwenye tizi la uwanjani litakaloanza leo Jumatatu ili kumpa nafasi Lwandamina kumteua mmoja aungane na wachezaji wengine kwa ajili ya msimu mpya.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
7h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
11h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
12h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
12h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
17h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’