Makocha wa klabu ya Simba wameueleza uongozi wa klabu ya Simba kwamba hawataki kusikia wanacheza mazoezi kwenye viwaja vibovu hali inayowaumiza vichwa viongozi wa Simba.
Mara kadhaa, makocha wamekuwa wakiwalazimisha kama si kuwakatalia viongozi viwanja vya mazoezi kwa kuwa havina ubora na vinasababisha majeraha kwa wachezaji.
Kaimu Rais wa klabu ya Simba, Abdallah Salim 'TryAgain' amesema kati ya mambo yanayowaumiza kichwa ni suala la Simba kukosa uwanja, lakini akasema mwezi huu haumaliziki kwa kuwa makocha wamekuwa wakiwasumbua.
Akizungumza na wahariri wa habari za Michezo jana Alhamisi, TryAgain alisema kuwa kuna suala la kesi ambalo liko mahakamani na hataki kulizunguzia na kwamba kwa mwelekeo wake, mambo yanaweza kufunguka na wakapata njia ya uwanja.
"Ninachotaka kusema ni kwamba watu wawe na subira, mwezi huu wa nane haumaliziki, tukimaliza Simba Day tunakwenda Bunju, hilo ndilo tunalotaka kulifanya kwa sasa, Simba klabu kubwa lazima kuwa na uwanja wake."
Amesema makocha hawataki kupeleka wachezaji kwenye baadhi ya viwanja kwa kuwa havina ubora na akasema viwanja vizuri ni gharama hivyo ni wakati sasa Simba kupunguza ama kuondoa gharama hizo kwa kujenga uwanja wa kisasa wa Bunju.
Simba imekuwa ikihangaika uwanja wa mazoezi na huwa inatumia Uwanja wa Boko Veterans kwa ajili ya mazoezi ambao hutozwa Sh300,000 kwa siku.
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE