Kikosi cha Yanga leo kimefanya mazoezi kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro kujiandaa na mchezo wa robo fainali kombe la FA dhidi ya Singida United.
Yanga iko Morogoro tangu jana ikijifua kikamilifu tayari kwa mchezo huo.
Kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina ameongeza 'dozi' ya mazoezi kuhakikisha wachezaji wake wanakuwa imara ili kutinga nusu fainali ya ASFC.
Naye Meneja wa Yanga Hafidh Saleh amesema wachezaji wote waliosafiri akiwemo Donald Ngoma wanaendelea vizuri na mazoezi.
Saleh amesema wachezaji wote wako vizuri na morali ya ushindi, hivyo kuongeza muda wa mazoezi kutachangia kwa kufanya vyema katika mchezo huo.
"Kikosi kipo vizuri, tayari Lwandamina ameongeza muda wa mazoezi badala ya mara mmoja sasa tutafanya mara mbili kwa siku asubuhi na jioni," amesema
Aidha baada ya kukamilika kwa mchezo wa kirafiki kati ya Tanzania dhidi ya DR Congo, wachezaji wa Yanga waliokuwa kwenye kikosi cha Stars wanatarajiwa kusafiri mkoani Morogoro kuungana na wenzao.
Wachezaji hao ni Ramadhani Kabwili, Hassani Kessy, Gadiel Michael, Kelvin Yondani na Ibrahim Ajib

ADVERTISE HERE