Uongozi wa Simba umewalaumu waamuzi wa Ligi Kuu Bara kwa kuchezesha vibaya mechi zao msimu huu.
Mapema leo, akizungumza na wanahabari katika makao makuu ya klabu ya Simba mtaa wa Msimbazi, Afisa habari wa klabu hiyo, Haji Manara alilalamikia waamuzi kuchezesha vibaya mechi zao.
Manara alisema katika mechi tatu za Simba mfululizo msimu huu waamuzi wamekuwa wakiwafanyia uamuzi ya uonevu dhidi yao tena akiwa katika mechi ya Mbao, Stand United na Yanga.
Manara alisema mechi dhidi ya Mbao mwamuzi alitoa penalti ambayo haikuwa sahihi kwani katika tukio hilo beki wao Ally Shomari hakuushika ule mpira bali ulimgonga kifuani.
Manara alisema mechi iliyofuata dhidi ya stand United walinyimwa penalti mbili ambazo zote zilikuwa halali baada ya mshambuliaji wao John Bocco kuchezewa rafu ndani ya eneo la hatari.
Katika mechi ya Yanga, Manara alisema mwamuzi Elly Sasii aliwanyimwa penalti mbili alikuwa karibu na eneo la matukio yote mawili lile la Papy Tshishimbi na Kelvin Yondan kushika mpira kwenye eneo la penalty.
Manara amesema tayari Simba imepeleka malalamiko rasmi kwa Bodi ya Ligi

ADVERTISE HERE