Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba saa kumi jioni wanashuka kwenye uwanja wa Taifa kucheza na APR katika mchezo wa pili kombe la Kagame, kundi C.
Mchezo wa mapema utakaoanza saa nane utakuwa kati ya Singida United dhidi ya Dakadaha FC.
Simba inaongoza kundi C ikiwa na alama tatu na mabao manne kufuatia ushindi wake wa mabao 4-0 dhidi ya Dakadaha kwenye mchezo wake wa kwanza.
Singida United nayo ina alama tatu na mabao mawili kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya APR.
Kama Simba itaifunga APR leo basi itakuwa imejihakikishia kutinga hatua ya robo fainali kabla ya kucheza na Singida United.
Kaimu Kocha Mkuu wa Simba Masudi Djuma amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo huo na ana matumaini makubwa kwa vijana wake kuibuka na ushindi.
Mshambuliaji mpya wa Simba aliyesajiliwa kutoka Gor Mahia Meddie Kagere huenda akawemo kwenye kikosi kitakachoshuka dimbani kwenye mchezo huo.

ADVERTISE HERE