Yanga bado iko Kusini mwa Tanzania ambapo baada ya mchezo wake wa kombe la FA dhidi ya Majimaji juzi, kesho Jumatano inashuka kwenye dimba la Nangwanda Sijaona Mtwara kuivaa Ndanda FC.
Jambo la kufurahisha ni mapokezi ya aina yake inayopatiwa timu hiyo maarufu kama 'timu ya wananchi'.
Licha ya kuwa ugenini, umoja na ushirikiano wa Wana Jangwani wa mikoani unafanya wachezaji, benchi la ufundi na viongozi walio kwenye msafara wajisikie wako nyumbani.

Hali iliyokuwa Ruvuma, ndiyo inayoonekana mkoani Mtwara ambako tayari Yanga imeingia kusubiri mchezo wa kesho.
Kama kawaida Wana Yanga wa Mtwara wameahidi kuujaza uwanja wa Nangwanda kuishangilia timu yao mwanzo mwisho kuhakikisha inaibuka na ushindi muhimu dhidi ya Ndanda FC.

ADVERTISE HERE