Kocha mkuu wa timu ya Simba Joseph Omog, amesema sare waliyoipata juzi dhidi ya Yanga, ilitokana na ubora waliokuwa nao wapinzani wao.
Shiza Kichuya ndio aliyekuwa wa kwanza kuifungia Simba bao la kuongoza lakini dakika tatu baadaye Obrey Chirwa, aliisawazishia Yanga na mchezo huo kumalizika kaa sare ya 1-1.
Omog amesema wachezaji wake walijitahidi kubadilisha kila mbinu lakini mbinu hizo zilishindikana kutokana na wachezaji wa Yanga kubaini na kuziba njia zote.
"Mchezo ulikuwa mgumu, na ndiyo maana matokeo yamekuwa hivi, Yanga, imeonyesha kuwa ni timu nzuri na ngumu kutokana na namna walivyocheza," alisema Omog.
Mcameroon huyo alisema matokeo hayo hayawakatishi tamaa ya kutwaa taji Hilo msimu huu na mipango yao kwasasa ni kuhakikisha wanashinda mechi zote zilizosalia kwenye mzunguko wa kwanza ili kujiweka mazingira mazuri ya kuwa mabingwa msimu huu.
Kocha huyo amesema ameridhika na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wake katika mchezo huo, na amesema kama wataendelea hivyoo matumaini ya kutwaa ubingwa ni makubwa sana

ADVERTISE HERE