Yanayojiri Urusi : Mbappe aipeleka Ufaransa robo fainali ya kombe la Dunia, yaifumua Argentina 4-3

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1 Jul 2018
Yanayojiri Urusi : Mbappe aipeleka Ufaransa robo fainali ya kombe la Dunia, yaifumua Argentina 4-3
Mshambuliaji kinda Kylian Mbappe ameisaidia Ufaransa kutinga robo fainali ya michuano ya kombe la dunia baada ya kufunga mabao mawili na kusababisha penati kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora dhidi ya Argentina ulioshuhudia mabao saba yakifungwa Ufaransa ikishinda kwa mabao 4-3.

Kasi ya Mbappe ilikuwa tatizo kubwa kwa walinzi wa Argentina ambapo kwenye dakika ya 13 alifanyiwa madhambi ndani ya 18 na Marcus Rojo na mwamuzi kuipa Ufaransa mkwaju wa penati uliowekwa kambani na Antoine Griezmann.

Hata hivyo Angel Di Maria aliirudisha Argentina mchezoni kwenye dakika ya 41 kwa kufunga bao safi baada ya kumtungua Hugo Lloris akiwa nje ya 18.

Kwenye kipindi cha pili Argentina ilitangulia kupata bao la pili kwenye dakika ya 48 kupitia kwa Gabriel Mercado aliyeunganisha shuti la Lionel Messi.

Kuingia kwa bao hilo kuliiamsha Ufaransa ambayo ilifunga mabao matatu ya haraka haraka kupitia kwa Pavard na mabao mawili ya Mbappe.

Argentina ilifunga bao la tatu kwenye dakika za majeruhi mfungaji akiwa Sergio Aguero lakini hakukuwa na muda zaidi wa kuweza kusawazisha.

Kiwango kilichoonyeshwa na Ufaransa kwenye mchezo kinaifanya kuwa miongoni mwa timu zinazoweza kutwaa taji la kombe la dunia huko Urusi.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
6h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’