Mashabiki wa Simba na Yanga wameendelea kuishi kwa mazoea wakisubiri kununua tiketi siku za mechi, jambo ambalo limesababisha mauzo ya tiketi za mchezo wa watani hao wa jadi kesho Jumamosi kukwama.
Simba na Yanga zinakutana kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam wenye uwezo wa kubeba mashabiki 22,000 tu, lakini mpaka majira ya saa 4.18 asubuhi ya leo Ijumaa ni tiketi 2,012 tu zilizouzika. Tiketi hizo zilianza kuuzwa Jumatatu ya wiki hii.
Mchezo huo wa watani wa jadi kwa mara ya kwanza baada ya miaka 10 unachezwa kwenye uwanja wa Uhuru ambao unawanyima fursa mashabiki 38,000 kuutazama ukilinganisha na ule wa Uwanja wa Taifa ambao ni mkubwa zaidi Afrika Mashariki na Kati.
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura alisema wanasubiri mpaka leo Ijumaa jioni kuona hali ya mauzo inakwendaje ili kuona kama kesho Jumamosi kutakuwa na usumbufu mkubwa kwenye ununuzi.
Kwa hisani ya Mwanaspoti

ADVERTISE HERE