Kuhusu swala la Niyonzima

Admin By Admin
β€’
15 Jul 2017
Kuhusu swala la Niyonzima
Kuna wadau wengi wamekuwa wakiuliza juu ya habari zinazodai kuwa aliyekuwa kiungo wa Yanga Haruna Niyonzima ameomba kurudi asaini mkataba Yanga, ngoja tuliweke sawa hili.

Uongozi umesisitiza kuwa mazungumzo na Niyonzima yalishafanyika na pande mbili zikashindwa kufikia makubaliano hivyo akaruhusiwa kuondoka kujiunga na timu yeyote anayotaka pale mkataba wake utakapomalizika siku chache zijazo.

Taarifa kuhusu uamuzi wa Yanga ilitolewa na Katibu Mkuu, Charles Mkwasa na kushauri mjadala juu ya Niyonzima umalizike.

Ukweli ni kwamba hakuna kilichobadilika kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa kwa nyakati tofauti na viongozi.

Niyonzima ni mchezaji mzuri na ameifanyia Yanga mambo makubwa hilo halina mjadala. Mashabiki wa Yanga walimpenda na hata sasa bado wanampenda.

Lakini ilikuwa ni uamuzi wake yeye mwenyewe kukataa kusaini mkataba mpya licha ya uongozi kufanya kila jitihada kumshawishi.

Ifahamike pia kuwa baada ya Yanga kutangaza kuachana na Niyonzima iliweza kufanya majadiliano na wachezaji wengine ili kuziba nafasi yake.

Sitarajii kwamba uongozi baada ya kushindwa kumshawishi ulikaa tu kusubiri muujiza eti labda atabadili mawazo.

Ni wazi kuna wachezaji walifanya mazungumzo na Yanga na inawezekana wachezaji hao wamesajiliwa tayari wanasubiri kutangazwa tu.

Hivyo mi nadhani itoshe kusema Yanga ni timu kubwa na haijawahi kutegemea mchezaji mmoja.

Haina haja ya kuhangaika na mchezaji mmoja wakati klabu imesajili wachezaji wazuri pengine zaidi yake.

Pia Niyonzima hakufukuzwa Yanga, aliamua kwa utashi wake kukataa kuongeza mkataba na hata akiamua kurudi viongozi wanaweza wakamfikiria lakini naamini hawezi kuwa kipaumbele cha klabu kwa sasa.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
4h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’