Mkuu wa Idara ya habari ya klabu ya Simba Haji Manara amesema wako tayari kwa ajili ya mchezo wa fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup dhidi ya Gor Mahia.
Mchezo huo utapigwa katika uwanja wa Afraha, Jumapili Juni 10 2018.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo, Manara amesema wanaheshimu uwezo wa Gor Mahia, lakini wamejipanga vizuri na wanaamini kutakuwa na mchezo mzuri kutoka kila upande.

"Tunawaheshimu Gor Mahia ila hatuwaogopi. Tuna imani kubwa mechi itachezeshwa kwa haki kwa sababu SportPesa ni kampuni kubwa yenye heshma duniani na wameandaa mashindano makubwa.
"Kilichobaki ni mashabiki na watanzania kutuombea na kuja kutushangilia. Sisi tupo tayari kwa mchezo wa Jumapili," amesema Manara.

Kwenye Mkutano huo, Manara aliongoza na wachezaji waandamizi wa kikosi cha Simba Shomari Kapombe na Aishi Manula ambao wote wameahidi Simba kuibuka na ushindi na kuweza kutwaa taji la SportPesa Super Cup keshokutwa

ADVERTISE HERE