Kocha KK HomeBoyz aihofia Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
6 Jun 2018
Kocha KK HomeBoyz aihofia Simba
Kocha mkuu wa Kakamega Home Boys ya Kenya, Paul Nkata amekiri mchezo wa nusu fainali wa michuano ya SportPesa Super Cup dhidi ya Simba kesho utakuwa mgumu kwao.

Nkata amesema anafahamu Simba ni mabingwa Tanzania, na wana historia nzuri katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Naye Kocha Msaidizi wa Simba Masudi akizungumza na Wanahabari katika Hoteli ya Ole-Ken jijini Nakuru, amesema wanaiheshimu KK HomeBoyz.

Lakini amesema wanahitaji kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo ili waweze kutinga fainali.

"Tulicheza vibaya mchezo uliopita, kila mmoja wetu ameliona hilo. Hatuwezi kurejea tena kwa akili hiyo. Wachezaji wote wameona tunahitaji kubadilika kwenye mechi ya kesho," amesema Djuma

Kwa upande wake nahodha wa Simba Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr' amesema watahakikisha wanapata ushindi kwenye mchezo wa kesho ndani ya dakika 90.

"Penalti siyo nzuri, ni kama bahati nasibu. Tulikuwa na mpango wa kushinda ndani ya dakika tukashindwa dhidi ya Sharks lakini tutarejea tukiwa tofauti ili tuweze kushinda," amesema Zimbwe Jr

KK HomeBoyz ndiyo iliyoiondosha Yanga kwenye michuano hiyo kwa kuilaza mabao 3-1 kwenye mchezo wa ufunguzi, Juni 03 2018.

Simba na Kaka HomeBoyz zitacheza kwenye mchezo wa kwanza wa nusu fainali utakaopigwa kwenye dimba la Afraha kesho Alhamisi, Juni 07 saa saba mchana kisha kufuatiwa na mchezo mwingine wa nusu fainali kati ya Gor Mahia dhidi ya Singida United.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’