FT : Lipuli 0-2 Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Feb 2018
FT : Lipuli 0-2 Yanga
Mabingwa watetezi ligi kuu ya Vodacom, Yanga leo wameondoka na alama zote tatu kwenye uwanja wa Samora baada ya kuilaza Lipuli FC mabao 2-0 katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 16.

Yanga ilihitaji kufanya kazi ya ziada kupata ushindi huo kwani wenyeji, Lipuli FC walikuwa wamekamia kuhakikisha wanawazuia mabingwa kwenye uwanja wao wa nyumbani.

Mchezo huo ulitawaliwa na ubabe pamoja na rafu za hapa na pale kutoka kwa wenyeji, Lipuli FC.

Mpira wa kona uliopigwa na Geofrey Mwashiuya kwenye dakika ya 19 kisha kuunganishwa kwa kichwa na Emanuel Martin, ulimshinda mlinda lango wa Lipuli FC na kumpa kazi rahisi kiungo Papi Tshishimbi aliyekuwa sehemu sahihi kuusukumizia wavuni na kuihesabia Yanga bao la kuongoza.

Katika kipindi cha kwanza Yanga ilipata pigo baada ya mlinda lango wake Youthe Rostand kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na kinda Ramadhani Kabwili.

Aidha katika kipindi cha kwanza mchezo huo haukuwa na ufundi mwingi, timu zote zilitumia zaidi mipira mirefu.

Kipindi cha pili Lipuli ilianza kwa kasi ikisaka bao la kusawazisha lakini ni Yanga iliyoongeza bao la pili kupitia shambulizi la kushitukiza mfungaji akiwa Pius Buswita.

Buswite alianzisha shambulizi hilo kwenye dakika ya 56 kwa kumtengea pasi murua Obrey Chirwa aliyeambaa mpaka kwenye eneo la hatari la Lipuli FC kisha kumjazia majaro Buswita aliyemramba chenga mlinda lango kisha kuutumbukiza mpira kimiani.

Licha ya mashambulizi mengi ya Lipuli yaliyoongozwa na mshambuliaji wa zamani wa Yanga Malimi Busungu, uimara wa safu ya ulinzi ya Yanga uliweza kulinda ushindi huo muhimu.

Yanga iliingia kwenye mchezo huo ikimkosa beki wake mwandamizi Andrew Vicent 'Dante' ambaye aliondolewa kikosini kutokana na majeruhi.

Aidha Yanga ilikuwa na uhaba hata kwa wachezaji wa akiba kabla Juma Mahadhi hajaongezwa baada ya daktari kujiridhisha kuwa anaweza kumudu mchezo.

Kuumia kwa Rostand kunaongeza idadi ya majeruhi kikosini huku ikiwa imesalia wiki moja tu kabla ya kuivaa St Louis kwenye mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
4h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
7h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’