Baada ya kutolewa ratiba ya michuano ya CECAFA Kagame Cup inayoanza Juni 28 2018, huku vilabu vya Simba na Yanga vikiwa vimepangwa kundi moja, Mkuu wa Kitengo cha Habari katika klabu ya Simba, Haji Manara ameitaka klabu ya Yanga 'isiingie mitini.'
Manara amesema hawatapenda kuona yale yaliyotokea Nakuru Kenya kwa Yanga kufanya ujanja ili iondoshwe mapema, yanatokea tena.
"Nawatuma nyie watangazaji wa @azamtvtz mkawaambie mabosi zenu waongee na Cecafa..kutupanga na mbute mbute kundi moja kagame cup wana maana gani?
"kwa jinsi walivyo taabani si tutapiga sita?au na hii wataumwaga kama walivyotukimbia huku kwenye Sportpesa super cup? @hashimibwe @pascal_kabombe @sportpesa," ameandika Manara kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.

ADVERTISE HERE