Omog ajivunia rekodi nzuri dhidi ya Yanga

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
24 Oct 2017
Omog ajivunia rekodi nzuri dhidi ya Yanga
Kocha wa Simba Joseph Omog, hakuna anachojivunia katika pambano la Jumamosi dhidi ya Yanga zaidi ya rekodi zake mbele ya mbingwa hao watetezi

Kikosi cha Simba kimewasili Visiwani Zanazibar tayari kwa kambi ya wiki moja kwa ajili ya kuwakabili watani zao wa jadi Yanga, lakini kocha wa timu hiyo Joseph Omog, amesema anakwenda kwenye mchezo huo akijivunia rekodi yake nzuri ambayo anaamini itambeba na kupata ushindi Jumamosi.

Omog amesema, anatambua kuwa Yanga ni timu nzuri lakini kikosi chake ni bora zaidi ya mabingwa hao watetezi ambao wanalifukuzia taji la nne mfululizo.

"Nimeifunga Yanga mara mbili na kutoka sare mechi moja katika mechi sita nilizocheza nao nikiwa kocha wa Simba, kwahiyo najivunia rekodi hiyo ambayo naamini itanibeba na kupata matokeo mazuri katika mechi ya Jumamosi na hata mechi nyingine za ligi na michuano mengine," amesema Omog.

Kocha huyo amesema kambi yao ya Zanzibar, itakuwa ni maalumu kwa ajili ya kuwaweka sawa wachezaji wake na kuwakumbusha yale mambo muhimu yatakao wasaidia kupata ushindi na kujilinda ili wasiweze kupoteza mchezo.

Amesema anawajua Yanga, lakini siyo timu tishio kwake kutokana na ubora wa safu ya ushambuliaji na ulinzi imara ambao ameuandaa dhdi ya mshambuliaji Ibrahim Ajibu anayeonekana kuwa moto wa kuotea mbali kutokana na aina ya mabao aliyofunga katika mechi zilizopita.

Mechi ambazo Omog ameshinda dhidi ya Yanga ni ya Ligi Kuu Bara msimu uliopita Simba ilipoibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Omog akaiongoza tena Simba kuifunga Yanga kwa penalti 4-2 kwenye Kombe la Mapinduzi, kabla ya kuibuka tena na ushindi wa penalti 5-4 kwenye Ngao ya Jamii msimu huu.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
7h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
7h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
10h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’