Ushindi dhidi ya Ndanda FC leo utaifanya Simba ifikishe alama 65 hivyo pengine kuhitaji alama moja tu kuweza kutwaa ubingwa wakati hali ikiwa tofauti kwa wapinzani wao walio nafasi ya pili kutoka chini.
Msimu huu zinashuka timu mbili pekee na Ndanda tayari iko nafasi ya 15 ikiwa na alama 23, kimahesabu wanaweza kushuka daraja msimu huu.
Hali hiyo inafanya mchezo baina ya timu hizo unaopigwa kwenye uwanja wa Taifa kuwa na umuhimu wa kipekee kwa kila timu.
Licha ya mazingira hayo, ni Simba inayopewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kutokana na ubora wake.
Zilipokutana kwenye mchezo wa kwanza mkoani Mtwara, Ndanda ilifungwa mabao 2-0 yote yakiwekwa kimiani na nahodha wa Simba John Bocco.
Simba haijapoteza mchezo msimu huu na kuna kila dalili inaweza kumaliza msimu bila ya kufungwa.
Imebakisha michezo minne dhidi ya Ndanda, Singida United, Kagera Sugar na Majimaji

ADVERTISE HERE