Lechantre awawashia taa nyekundu Mzamiru, Mo, Ndemla

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
5 May 2018
Lechantre awawashia taa nyekundu Mzamiru, Mo, Ndemla
Wakati ligi kuu ya Vodacom ikielekea ukingoni na Simba ikiwa inahesabu siku tu kutawazwa mabingwa, kocha mkuu wa timu hiyo Pierre Lechantre tayari ameanza mikakati ya kukisuka kikosi chake kwa ajili ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu ujao.

Ubingwa utaifanya Simba ishiriki michuano hiyo na mabosi wa klabu hiyo hawataki kushiriki tu, wanataka kuiona Simba angalau ikitinga hatua ya makundi.

Taarifa za uhakika ni kwamba Lechantre amewatahadharisha wachezaji wake kuhakikisha wanaongeza bidii ili wasije wakaondolewa kikosini.

Lechantre ameeleza kutoridhishwa na viwango vya viungo wake washambuliaji Mzamiru Yassini, Said Ndemla, Mohammed Ibrahim, Mwinyi Kazimoto na Haruna Niyonzima.

Wachezaji hao wamekuwa hawapati nafasi kwenye kikosi cha Simba ambapo kwa nyakati tofauti Lechantre amekuwa akiwatumia Shomari Kapombe na Asante Kwasi katika namba zao.

Wakati Ndemla mkataba wake ukiwa tayari umemalizika na akielezwa anataka kutimkia Sweden, Mzamiru, Mo na Kazimoto mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu na hatma yao iko mikononi mwa Lechantre.

Mkataba wa Niyonzima unamalizika mwishoni mwa msimu ujao.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
5h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
23h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’