Kotecha awanyooshea mikono Okwi, Bocco

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
24 Apr 2018
Kotecha awanyooshea mikono Okwi, Bocco
Straika wa Mbao FC, Rajeshi Kotecha amesema moto wa nyota wa Simba, Emanuel Okwi na John Bocco si wa mchezomchezo na hakuna wa kuuzima na mastaa hao wamempa somo kubwa.

Okwi raia wa Uganda, tayari amefunga mabao 19, huku Bocco akiweka kimiani mabao 14 na Obrey Chirwa wa Yanga akifuata kwa mabao 12.

Kotecha alisema kasi ya Okwi na Bocco si ya mchezo kwani wameonyesha uwezo wa hali ya juu pamoja na ukongwe wao lakini bado wako vizuri.

“Ni wachezaji wakongwe kwenye Ligi Kuu lakini wamekuwa wakijituma uwanjani hili ni somo kubwa kwetu sisi washambuliaji chipukizi, kikubwa ni kujituma kwenye mazoezi hadi uwanjani,” alisema Kotecha.

Straika huyo alisema mbali na wakali hao wa Simba, lakini pia kiungo, Pius Buswita wa Yanga naye anamuweka kwenye orodha ya wachezaji bora hadi sasa.

“Mtu asikudanganye, Okwi na Bocco ni habari nyingine, lakini kwa Yanga Buswita ndiye mkali na akiendelea hivi, atafika mbali kwa sababu ana uwezo,” alisema straika huyo.

Kinda huyo mwenye mabao mawili hadi sasa, alisema alitarajia kuwa miongoni mwa wachezaji wa kuwania kiatu cha mfungaji bora, lakini kutokana na kutocheza mechi nyingi amewaachia vita hiyo kwa wenye uwezo.

“Nimecheza mechi chache, kama nane hivi na nimefunga mabao mawili tu hadi sasa, lakini nilitamani sana kupambana kutwaa kiatu cha mfungaji bora, lakini naona nimeshakwama,” alisema

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
9h ago
READ MORE →
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
11h ago
READ MORE →
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
13h ago
READ MORE →
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
14h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →