VPL yaendelea leo, Azam FC yabanwa mbavu Mbeya, Stand yaifumua Njombe Mji 3-1

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
9 Apr 2018
VPL yaendelea leo, Azam FC yabanwa mbavu Mbeya, Stand yaifumua Njombe Mji 3-1
Ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 23 imeendelea leo kwa michezo minne kupigwa katika viwanja tofauti.

Mkoani Mbeya, wenyeji Mbeya City wametoshana nguvu na Azam FC kwa kutoka suluhu ya bila kufungana.

Matokeo hayo yanazidi kufifisha ndoto za ubingwa kwa klabu ya Azam FC ambayo inaendelea kubaki nafasi ya tatu licha ya kucheza michezo miwili zaidi ya Simba na Yanga ikiwa na alama 45.

Stand United imeendelea kuiweka Njombe Mji katika hatari ya kuteremka daraja baada ya kuifumua mabao 3-1.

Nayo Ndanda FC imelazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Kagera Sugar, Mrisho Ngasa akiisawazishia Ndanda baada ya bao la Abdallah Mguhi wa Kagera Sugar.

Ruvu Shooting na Tanzania Prisons zimetoshana nguvu kwa kutoka suluhu ya bila kufungana.

Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kuendelea kesho Jumatatu ambapo mchezo mmoja utapigwa mkoani Morogoro, Mtibwa Sugar ikiwakaribisha vinara wa ligi hiyo Simba.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
9h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
13h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’