Msimu huu kiungo mshambuliaji Deus Kaseke ameshiriki michezo 18 kati ya 23 ambazo Yanga imecheza kwenye ligi
Ameanza katika michezo 12, ni mechi mbili tu ambazo alifanikiwa kumaliza dakika 90
Jumla ya michezo nane, Kaseke amecheza sio zaidi ya dakika 60
Ndiye kinara wa kuzifumania nyavu akifunga mabao sita na kutoa pasi nne za mabao
Kwa takwimu zake, nadhani kuna mahali Yanga ingefanya vizuri zaidi kama Kaseke angeaminiwa na kupewa muda zaidi wa kucheza
Kuna wakati Kaseke na Yacouba walitengeneza 'pacha' ya hatari lakini baada ya Yacouba kupata majeraha ni kama Cedric Kaze akapoteza imani kwa Kaseke
Kaseke ni sawa na 'jembe kuu kuu' ambalo kuna wakati halionekani kuwa na makali, lakini ndilo linalochimbua visiki vingi
ADVERTISE HERE