Mukoko awapa somo wachezaji Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Mar 2021
Mukoko awapa somo wachezaji Yanga

Kiungo na mmoja wa Manahodha wa Yanga Mukoko Tomombe amesema mabadiliko ya benchi la ufundi hayatakuwa na maana yoyote kama wao wachezaji wataendelea kucheza kwa mazoea

Mukoko aliyejumuishwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya DR Congo, amesema pamoja na mbinu za Mwalimu, wao wachezaji ndio wenye jukumu la kuamua matokeo ndani ya uwanja

"Yanga ni klabu kubwa, inapopoteza mashabiki wengi wanaumia. Sina tatizo kama uongozi utakuwa umefukuza makocha najua watakuja wengine hayo ndio maisha lakini kuna kitu kama wachezaji lazima tubadilike," alisema Mukoko

"Bado wengi hatupo kwenye ubora wa ushindani hii ni klabu kubwa lazima uwe na moyo mgumu wa kuchezea klabu kama hii,tunatakiwa kuelewa hapa kuna presha watu wanataka ushindi hata kama tukipoteza isiwe kirahisi kama ilivyokuwa hivikaribuni"

"Hatuwezi kukimbia sasa tumeshasaini mkataba muhimu ni kuamua kubadilika, yapo makosa ambayo hata makocha walioondoka walikuwa wanatukumbusha lakini bado tukayafanya"

"Nafahamu mpira ni mchezo wa makosa lakini tunatakiwa kupunguza makosa kuthibitisha sisi ni wachezaji wenye hadhi ya kuichezea Yanga, kuna mechi moja inanikumbusha mengi tulipocheza na Prisons kule kwao (Sumbawanga). Hatukukubali kupoteza kirahisi hata kama tulikutana na mazingira magumu tunatakiwa kucheza kwa ubora ule katika mechi zote, angalia hata mechi ya wenzetu (Simba) walifanya makosa lakini walipambana hadi mwisho na kuambulia sare"

"Kama tukiamka kama wachezaji na kujitambua tutawasaidia makocha wanaokuja,viongozi na hata mashabiki wetu jukumu hili lipo kwetu kama wachezaji, hatuwezi kukata tamaa"

"Hata wao (Simba) walijua kwamba watashinda lakini mambo hayakua hivyo ilikuwa pointi 7 na sasa zimerudi tano na ligi bado haijamalizika, hii inaniambia bado tuna nafasi ya kupata kitu msimu huu kama mambo yetu tutayabadilisha haraka," Mukoko alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
5h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’