Bumbuli ampa somo Macha

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Mar 2021
Bumbuli ampa somo Macha

Afisa Habari wa klabu ya Yanga Hassan Bumbuli amemtaka Mwanahabari Gift Macha ambaye anafahamika kuwa mdau wa klabu ya Simba aache kupotosha umma kupitia tukio la Mtendaji wa Simba Barbara Gonzalez kusafiri Morocco kushuhudia uchaguzi wa kumpata Rais wa CAF uliofanyika jana

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Gift alihoji kwa nini Senzo hakufanya ziara nje ya nchi wakati yuko Simba na sasa akiwa Yanga

"Mdogo wangu Gift Macha kuna mambo unapaswa kufahamu, najua unayajua ila unajitoa ufahamu kwa sababu zako binafsi"

"Hapa umemtaja Senzo kwamba hakusafiri, sasa Senzo aliajiriwa kama football expert kutoka nje ya nchi, Simba waliamini katika uwezo wake, (rejea press ya utambukisho ya Senzo, akielezewa na Magori) sasa ulitaka asafiri akajifunze nini?"

"Kwa CV ya Senzo kwenye mpira wa Afrika anahitaji kwenda kupiga picha na viongozi wa CAF au FIFA kama hana shughuli?"

"Unashindwa kuandika ukweli kwamba huyo Babra ni mchanga kwenye mpira hajui lolote hivyo anakwenda kujifunza walau aweze kuongea lugha ya mpira as CEO, unabaki kushambulia watu kwa facts rahisi na za kipuuzi"

"Yaani Yanga tumlipie Senzo kwenda Morocco while tukijua si Mjumbe wa mkutano na hakuna seminar ya kujifunza kitu Kipya yaani aende tu akashangae watu, akapigepige picha na watu maarufu halafu tuwarushe roho watu kwenye mitandao kweli?"

"Bro hata kama ni fedha mnalipwa basi ipe Digirii yako thamani," aliandika Bumbuli

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’