Shirikisho la soka duniani (FIFA), limefuta pingamizi la kumzuia kocha wa zamani wa Yanga Luc Eymael kufanya kazi Afrika Kusini
Mwishoni mwa mwaka jana chama cha soka cha Afrika Kusini (SAFA), kilimzuia Eymael kujiunga na timu ya Black Leopards kutokana na matamshi ya kibaguzi aliyoyatoa wakati akiinoa klabu ya Yanga
Yanga na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) waliwasilisha malalamiko FIFA kutokana na matamshi ya kocha huyo
Afrika Kusini ilimzuia Eymael kujiunga na Black Leopards nae kupeleka malalamiko FIFA akipinga kufungiwa
Katika utetezi wake, Eymael alisema maneno aliyotamka hayakulenga ubaguzi wowote, tafsiri ndiyo iliyopotoshwa
ADVERTISE HERE