Mortotsi alivyonusurika na panga la Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
12 Mar 2021
Mortotsi alivyonusurika na panga la Yanga

Jana ziliibuka taarifa kuwa kocha wa viungo Edem Mortotsi amerejeshwa kuendelea na majukumu yake

Mortotsi alikuwa miongoni mwa waliotemwa  baada ya uongozi wa Yanga kutangaza kulivunja benchi lote la ufundi lililokuwa chini ya kocha Cedric Kaze

Kocha huyo raia wa Ghana, alijiunga na Yanga mwezi uliopita akitokea nchini Canada

Afisa habari wa Yanga Hassan Bumbuli amethibitisha kurejeshwa kwa Mortotsi huku akieleza sababu iliyopelekea arudishwe kuwa ni baada ya kubaini hakuwa na kosa lolote kwani hakuwa na zaidi ya siku 30 tangu alipojiunga na Yanga

"Uongozi umekaa na kuamua kumrudisha kocha wa viungo Mortotsi, sababu hawakuona kosa lolote kwenye idara yake hivyo kwa sasa ataendelea na ajira yake akisaidiana na Mwambusi tukiamini ataendeleza yale ambayo tulikuwa tunayatarajia kutoka kwake," alisema Bumbuli

Bumbuli amesema mchakakato wa kumpata kocha mpya atakayeinoa timu hiyo unaendelea vizuri na pengine wiki ijayo wanaweza kuwa na jina la kocha mpya

Alisema wamepokea CV za makocha wengi kutoka mataifa mbalimbali na wanachokifanya hivi sasa ni kuzipitia kwa makini ili kupata kocha bora atakaye ipa timu yao mafanikio katika mbio za Ligi Kuu zinazoendelea hivi sasa

Kocha Msaidizi Juma Mwambusi ambaye kwa sasa anakaimu nafasi ya kocha mkuu, alianza rasmi majukumu yake hapo jana akisaidiana na Mortotsi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE →
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE →