Kikosi cha Yanga leo Jumapili, Disemba 17 kinashuka kwenye uwanja wa Uhuru kuumana na timu ya Jeshi la Polisi la Tanzania katika mchezo wa kirafiki.
Mchezo huo ni sehemu ya maandalizi ya kikosi cha Yanga kinachokabiliwa na michezo miwili kuelekea mwishoni mwa mwaka.
Yanga wiki ijayo itachuana na Reha FC kwenye mchezo wa kombe la FA mzunguuko wa kwanza kabla ya kushuka tena dimbani Disemba 31 kuuumana na Mbao FC ugenini katika mchezo wa mzunguuko wa 12 ligi kuu ya Vodacom.
Baada ya michezo hiyo Yanga itaelekea visiwani Zanzibar kushiriki kombe la Mapinduzi.
Kocha Msaidizi Shedrack Nsajigwa anatarajiwa kuwaongoza vijana wake leo kwani Kocha Mkuu George Lwandamina amekwenda kwao nchini Zambia kuhudhuria shughuli ya kifamilia.
Bila shaka wachezaji wapya waliosajiliwa na Yanga wakati wa dirisha dogo la usajili, beki Fiston Kayembe na Yohana Mkomola watapata nafasi ya kuonekana na mashabiki wa Yanga kwa mara ya kwanza.
Kadhalika mshambuliaji Amissi Tambwe ambaye hajaichezea Yanga kwa zaidi ya miezi minne anatarajiwa kurejea dimbani leo.

ADVERTISE HERE