Leo ilikuwa siku ngumu sana kwa wachezaji wa Yanga ambao walipata wasaa wa kuagana na kocha Cedric Kaze
Kaze amemalizana na uongozi wa Yanga leo na yuko tayari kuondoka nchini baada ya miezi mitano ya kuitumikia Yanga kufikia tamati
Kocha huyo raia wa Burundi, amesema anajivunia muda aliofanya kazi Yanga, akiamini ameacha kitu cha kukumbukwa miongoni mwa wachezaji na mashabiki
"Unapowaacha wachezaji wako na huzuni, ndipo unagundua mafanikio yanapimwa tu kwa vile ulivyowainua wengine," Kaze aliandika ujumbe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Kwa hakika Kaze atakumbukwa kwa kile alichofanya japo kwa wengine kinaweza kuonekana ni kidogo
Ni kocha aliyejitoa sana, muda mwingi akiutumia kazini katika majukumu yake aliyokuwa nayo Yanga
Β
ADVERTISE HERE