Kabla ya michezo miwili ya kuwania kufuzu fainali za michuano ya Afcon dhidi ya Guinea ya Ikweta na Libya, kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kinatarajiwa kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Kenya
Kulingana na ratiba iliyotolewa na TFF, March 15, Tanzania itakuwa nchini Kenya kuwakabili wenyeji wao Harambee Stars katika mchezo wa Kimataifa wa kirafiki
Timu hizo zitarudiana tena March 18. Baada ya mchezo huo Tanzania itaelekea Guinea ya Ikweta kwa ajili ya mchezo wa raundi ya tano dhidi ya wenyeji wao utakaopigwa March 25

Baadae Tanzania itarejea nyumbani kukamilisha mchezo wa mwisho hatua ya makundi dhidi ya Libya, March 28
Tanzania inashika nafasi ya tatu kundi J ikiwa na alama nne nyuma ya Guinea ya Ikweta yenye alama sita na Tunisia yenye alama 10
Stars inapaswa kuhakikisha inashinda mechi hizo ili kujihakikishia nafasi katika michuano ya Afcon 2021 kwa mara ya tatu
Stars tayari imeingia kambini chini ya kocha Kim Poulsen aliyetua hivi karibuni kuchukua nafasi ya Etienne Ndayiragije