Sijawahi kumpigia simu Metacha - Dk Msolla

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Mar 2021
Sijawahi kumpigia simu Metacha - Dk Msolla

Miongoni mwa masuala ambayo Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla aliyatolea ufafanuzi wakati akizungumza na wanahabari jana, ni kuhusu tuhuma za kumpigia simu mlinda lango Metacha Mnata baada ya mchezo dhidi ya Polisi Tanzania uliomalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1

Simu hiyo ndio inayodaiwa kumvuruga Metacha ambaye jana aliweka ujumbe wa kuwaaga mashabiki wa Yanga lakini baadae akaondoa ujumbe huo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii

Dk Msolla amesema hakumpigia simu Metacha na hana kawaida ya kuwapigia simu wachezaji moja kwa moja

Amesema kilichotokea kuna watu wenye nia ovu walitumia namba yake kupiga simu mlinda lango huyo kakini si yeye

"Mimi sina kawaida ya kuwapigia simu wachezaji moja kwa moja. Kama kuna jambo napendelea kuzungumza na Mameneja wao. Jana baada ya kupewa taarifa ya ujumbe wa Metacha, nilimtafuta Meneja wake (Jemedari Said), sikuweza kumpata lakini leo nimezungumza nae kwa kirefu"

"Kimsingi mimi sikupiga simu hiyo, kuna watu walitumia namba yangu ya simu (walihack) wakapiga simu na kutoa tuhuma zao. Hata ukienda TCRA kufuatilia taarifa za mawasiliano ya namba yangu, hutaona kama mimi nimepiga simu kwa Metacha"

"Hizi ni vita, sijui aliyefanya jambo hili alikusudia nini lakini mimi sijawahi kuzungumza na mchezaji mmoja mmoja. Siku zote huwa naenda kambini na kama kuna jambo nitazungumza na wachezaji wote kama kundi," alisema Dk Msolla

Dk Msolla amesema atakutana na Metacha kuzungumza nae kuhusu suala hilo kuwa hahusiki kwa namna yoyote

Ni wazi lipo kundi la watu linafanya jitihada kuhakikisha wanaivuruga Yanga na kama Wanayanga wasipokuwa makini, lengo lao litafanikiwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
19h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’