Mwambusi anaweza kurudi Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Mar 2021
Mwambusi anaweza kurudi Yanga

Wakati uongozi wa Yanga ukiendelea na mchakato wa kusuka upya benchi la ufundi, aliyekuwa kocha msaidizi wa timu hiyo Juma Mwambusi huenda akarejeshwa kuiongoza timu hiyo wakati mchakato ukiendelea, imefahamika

Mwambusi aliondoka Yanga baada ya kumalizika michuano ya kombe la Mapinduzi, uongozi ukimruhusu baada ya mwenyewe kuomba aende akatibiwe maradhi ya jino yaliyokuwa yakimsababishia maumivu ya kichwa

Mwambusi alifanyiwa upasuaji Hospitali ya taifa ya Muhimbili, hivi karibuni akinukuliwa na gazeti moja akisema kuwa amepona na yuko tayari kurejea Yanga kuendelea na majukumu yake

Mwambusi ndiye aliyekabidhiwa kikosi cha Yanga mwanzoni mwa msimu kabla ya ujio wa kocha Zlatko Krmpotic

Aliendelea kubaki hata kocha huyo alipotimuliwa na alishirikiana vyema na kocha Cedric Kaze kabla ya kupata changamoto iliyomfanya aondoke

Faida kubwa ambayo Mwambusi anayo ni kuwa anawafahamu wachezaji wote wa Yanga, amefanya nao kazi na pengine yeye ndiye aliyekuwa sababu ya Yanga kufanya vizuri katika mechi za duru la kwanza VPL kwani alipoondoka tu, ndio mambo yakaharibika

Upo uwezekano mkubwa Mwambusi atajumishwa katika benchi jipya la ufundi linalotarajiwa kuundwa akiendelea na majukumu yake ya kocha msaidizi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
11h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
15h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’