Ujumbe wa Metacha wazua taharuki

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Mar 2021
Ujumbe wa Metacha wazua taharuki

Jana kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, mlinda lango Metacha Mnata aliwashukuru mashabiki wa Yanga kwa sapoti na ushirikiano waliompa katika kipindi cha miaka miwili huku akiwatakia kila la kheri na mafanikio mema

Ujumbe huo ulizua taharuki kwenye mitandao ya kijamii kwani ni kama Metacha alikuwa akiwaaga Wanayanga

Hata hivyo Metacha aliuondoa ujumbe huo kwenye ukurasa wake baada ya muda mfupi

Tangu juzi uongozi wa Yanga ulivyovunja benchi lote la ufundi, wameendelea na vikao vya ndani

Zipo tuhuma za hapa na pale ambazo baadhi ya wachezaji wametuhumiwa kutokana na viwango vyao katika michezo iliyopita

Jana Yanga iliweka wazi kuwa wamezungumza na wachezaji, wanachunguza wale ambao watabaini kwa namna yoyote wanahusika kuhujumu timu basi hawatasita kuwachukulia hatua

Ukweli ni kwamba hakuna anayefurahishwa na mwenendo wa Yanga, uamuzi wa kumtimua kocha Cedric Kaze na benchi lake la ufundi haukuchukuliwa hivihivi

Ni baada ya kujiridhisha kuwa yapo mambo hayako sawa, hivyo halitakuwa jambo la kushangaza kusikia hata upande wa wachezaji baadhi yao nao wakaingia matatani

Hiki ni kipindi ambacho Wanayanga wanapaswa kuwa wamoja, wawaache viongozi wao wafanye kazi, kwani jambo lolote litakaloamuliwa, litawekwa hadharani

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’