Serikali imevitaki vilabu vya soka nchini kuhakikisha wasemaji wao wanazingatia maadili ya kuwa msemaji kama vile taaluma ya habari inavyoelekeza
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dk. Hassan Abbas, amesema Serikali imetoa mafunzo kwa wasemaji na maafisa habari wa vilabu vya soka nchini hivyo wanatarajia kuona mabadiliko
"Wasemaji ninaowaongoza wazingatie kuna maadili ya kuwa Msemaji kama vile taaluma ya habari ambayo inatuongoza, tumeshatoa mafunzo kwa Wasemaji wa Vilabu vya Mpira, tumeona kuna changamoto kweli wakati mwingine badala ya kuhamasiha Watu kwenda viwanjani unakuta Msemaji anahamasisha vurugu, Msemaji anasema Watu fulani wasije uwanjani ukija tutakutoa," amesema Dk. Hassan Abbas
“Wasemaji wafahamu usemaji sio kuropoka, usemaji una maadili yake, tumeshatoa mafunzo kwa Wasemaji wa Vilabu vyote vya michezo mbalimbali, huku tunakokwenda tunataka kuona mabadiliko. kwahiyo ni muhimu kwa Viongozi na Vyama vya Michezo kuhakikisha Wasemaji wao sio waropokaji isipokuwa ni Watu wanatimiza wajibu wa kitaaluma na kikatiba lakini sio porojo na uropokaji"