Uongozi wa klabu ya Yanga umewaruhusu wachezaji wake nane kujiunga na kambi ya timu ya Taifa, 'Taifa Stars' ambayo inatarajiwa kuingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mechi za kuwania kufuzu michuano ya Afcon
Hata hivyo Yanga imeliomba Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kumuchia beki Dickson Job ambaye ni majeruhi
"Tumetoa ruhusa rasmi kwa wachezaji wetu wote walioitwa , lakini tumeomba Dickson Job baada ya kuripoti wamruhusu kurejea kwenye klabu ili aendelee na matibabu kwa kuwa bado hajapona vizuri na anaendelea na programu ya matibabu," amesema Meneja wa Yanga Hafidhi Saleh
"Job bado hajakaa sawa ndiyo maana huku Yanga hajaanza kutumika katika mechi za Ligi na pia hajaingia kwenye programu ya mazoezi moja kwa moja"
"Madaktari wetu wamefanya mawasiliano na madaktari wa timu ya Taifa juu ya suala hilo, lakini kwa utaratibu tumemruhusu akajiunge na kambi kisha kama wataafikiana nasi watamuondoa Timu ya Taifa arejee kwetu aendelee na matibabu yake"
Wachezaji wa Yanga walioitwa Taifa Stars ni Metacha Mnata, Yassin Mustapha, Bakari Mwamnyeto, Dickson Job, Feisal Salum, Deus Kaseke, Ditram Nchimbi na Farid Mussa