Uongozi wa Yanga umefikia makubaliano ya kuachana na kocha Cedric Kaze na benchi lake la ufundi baada ya mfululizo wa matokeo mabaya
Kaze amewajibishwa kama bosi wa benchi la ufundi, ameshindwa kufanya kile kilichotarajiwa
Msimu huu Yanga imeweka malengo makubwa ya kushinda ubingwa, kwa matokeo aliyopata katika michezo sita iliyopita, ni wazi hawezi kufanikisha lengo hilo
Kaze ni kocha mzuri ambaye alihitaji muda mrefu kuweza kutengeneza timu imara, muda huo hawezi kuupata wakati huu ambao Yanga ina presha kubwa ya kusaka mafanikio
Uongozi wa Yanga umesikia maoni ya Wanachama na Mashabiki wake, tutarajie benchi la ufundi ambalo litasheheni makocha wenye uzoefu wa ligi kuu ya Vodacom
Yanga imeahidi kutangaza benchi jipya la ufundi haraka iwezekanavyo
Ni wakati sahihi Yanga kufanya mabadiliko hayo ya dharura kwani ligi itasimama kuanzia March 10 kupisha mechi za kufuzu fainali za Afcon
Kutakuwa na takribani wiki tatu ambazo benchi la ufundi wanaweza kutumia kukiweka sawa kikosi kabla ya ligi kuendelea mwezi April