Ni droo nyingine kwa Yanga, Wananchi wameacha alama nyingine mbili Arusha baada ya kukubali kulazimishwa matokeo ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid
Kwa mara nyingine, jitihada za kulinda ushindi wa bao 1-0 zilikwamishwa na bao la dakika ya 90 lililowekwa kambani na nyota wa zamani wa Yanga, Pius Buswita
Fiston Abdul Razak ndiye aliyetangulia kuifungia Yanga bao la kuongoza kwenye dakika ya 42 akimalizia krosi ya Tuisila Kisinda
Bado kocha Cedric Kaze na benchi lke laa ufundi wana kazi ya kufanya kukirejesha kikosi kwenye ari ya ushindani
Yanga iliyocheza duru ya kwanza sio hii inayoteseka kusaka matokeo mbele ya timu ambazo walipaswa kuzifunga kwa urahisi
Kabla ya kuzungumzia ubingwa, kwa hakika ipo kazi kubwa inapaswa kufanywa