Nahodha Lamine Moro anaweza kukosa mchezo dhidi ya Polisi Tanzania baada ya kupata majeraha katika mchezo uliopita dhidi ya Coastal Union
Mshambuliaji Michael Sarpong naye aliumia katika mchezo uliopita, leo hatarajiwi kuwemo katika mtanange huo
Lakini habari njema ni kurejea kikosini kwa Ditram Nchimbi aliyekosekana katika mchezo uliopita
Kocha Cedric Kaze leo anapaswa kuchanga karata zake vyema ili kuhakikisha Yanga inaondoka na alama zote tatu mkoani Arusha
Matokeo tofauti na ushindi, yanaweza kumuweka kwenye presha kubwa
Wananchi leo watatamani kumuona Deus Kaseke, kinara wa mabao akianza katika mchezo huo
Kiungo Haruna Niyonzima na Yacouba Songne pia wanaweza kujumuishwa katika kikosi cha leo
Eneo la safu ya ulinzi nalo linaweza kushuhudiwa mabadiliko Abdallah Shaibu na Said Juma Makapu wakipigiwa chapuo kuanza
Makapu na Ninja walifanya vizuri katika michuano ya kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar wakiisaidia Yanga kuibuka na ubingwa
Yanga leo inahitaji kuingia katika mchezo huo ikiwa na 'nguvu mpya' kuhakikisha wanapata matokeo