Kwa hakika Yanga inamuhitaji sana kiungo mshambuliaji Saido Ntibazonkiza ambaye yuko nje tangu mwezi Januari mwaka huu
Bado haijafahamika ni lini nyota huyo raia wa Burundi atarejea kikosini, ilielezwa kuwa alianza mazoezi mepesi siku chache kabla Yanga kusafiri kwenda Tanga
Ntibazonkiza ndiye aliyekuwa nyota wa kikosi cha Yanga mwezi Disemba 2020, mechi tatu alizocheza katika mwezi huo, zilitosha kumpa tuzo ya mchezaji bora wa VPL Disemba
Alifunga mabao mawili na kutoa pasi tatu za mabao baadae akapata majeraha ambayo yamemuweka nje mpaka sasa
Alilazimika kushiriki mchezo wa fainali ya kombe la Mapinduzi dhidi ya Simba kule visiwani Zanzibar pamoja na kuwa majeruhi
Uwepo wake ulikuwa chachu kwa Yanga kushinda kupitia mikwaju ya penati na kuibuka mabingwa

Wakati huu ambao timu inasuasua, mchezaji kama Ntibazonkiza alihitajika kuibeba timu kupitia uwezo wake binafsi
Ndio, zipo nyakati uwezo wa mchezaji mmoja mmoja unahitaji kuivusha timu katika kipindi kigumu
Matumaini ya Wanayanga ni kuona Ntibazonkiza anarejea kikosini haraka
Uongozi wa Yanga na wadhamini GSM wamefanya jitihada kuhakikisha Ntibazonkiza anarejea kikosini haraka