Kupitia ukurasa wa Mtandao wa Kijamii, Mjumbe wa kamati ya Utendaji klabu ya Yanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi, Dominick Albinus, amewataka mashabiki wa Yanga kuwa watulivu kwani kufungwa na Coastal Union sio mwisho wa msimu
Ameandika haya;
Katika maisha dhambi kubwa na kisa kubwa ni kukata tamaa, wananchi tuna utamaduni wa kutokukata tamaa na mara zote inapotokea changamoto hukaa chini kutafakari na kuamua kuanza upya kuyafuata mafanikio
Timu yetu bado iko katika mipango na mikakati ambayo haijatoweka tangu kuanza kwa ligi. Maapmbano bado yanaendelea na kilichotokea ni sehemu ya mchezo
Tulishapitia katika nyakati ngumu huko nyuma ambazo tulituliza akili na kuinuka upya mpaka tukafika hapa tulipo.
Timu iko vizuri, kocha mzuri, wachezaji wazuri na hivyo bado tuna imani ya kufikia malengo. Kupanda na kushuka hutokea kwa yeyote na timu yeyote, hebu tuangalie mifano michache tu ambayo hutokea hata kwenye nchi za walipiga hatua zaidi yetu.
Iko wapi Liverpool? Iko wapi Barcelona? Iko wapi Madrid? Mashabiki wao wanazidi kuziunga mkono timu zao na viongozi wao huku wakiamini ipo siku mambo yatakaa vizuri na kurudi katika hali yao ya kawaida.
Yanga ni ndiyo timu pekee katika ligi yetu kupoteza mechi moja tu na pia ndiyo timu pekee katika ligi kushinda mechi nyingi ugenini ikifanya hivyo mara saba,bado inaongoza msimamo wa ligi, hofu inatoka wapi?
Ni nani ametudanganya kuwa ukifungwa huchukui ubingwa? Tutulie tuendelee kuiunga mkono timu yetu ili tutimize malengo ya kutwaa ubingwa wa VPL
Shime wananchi tuendelee kushikamana na kuiunga mkono timu yetu kwa kujaa kwa wingi uwanjani ili kuwatia moyo wapambanaji wetu
Daima mbele nyuma mwiko