Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze amesema vijana wake jana hawakuwa katika kiwango bora, hivyo wamekubali wamepotez mchezo kihalali dhidi ya Coastal Union
Coastal Union ilishinda mabao 2-1 jana na kuwa timu ya kwanza kupata ushindi dhidi ya Yanga msimu huu
Akizungumza baada ya mchezo huo uliopigwa uwanja wa Mkwakwani, Kaze amesema makosa waliyofanya yamewagharimu
"Hatukuwa vizuri, Coastal Union walicheza vizuri zaidi nawapongeza kwa kupata ushindi. Utaona tulianza mchezo taratibu, wapinzani wetu walikuwa wanashinda kila tukio la kugombea mpira"
"Kipindi cha pili tulikuwa na tatizo katikati, wakati tukienda kushambulia tuliacha uwazi eneo la kiungo, wapinzani wetu walitumia makosa hayo"
"Siwezi kulaumu ubora wa uwanja kwa kuwa sote tulicheza katika uwanja huo. Itoshe kuwapongeza wapinzani wetu kwani walikuwa bora zaidi yetu," alisema Kaze
Yanga ina siku tatu za kusahihisha makosa kabla ya mchezo unaofuata dhidi ya Polisi Tanzania utakaopigwa Jumapili uwanja wa Sheikh Amri Abeid