Kiungo wa Yanga Carlos Carlinhos amesema wamekubali kupoteza mchezo dhidi ya Coastal Union kwa kufungwa mabao 2-1 lakini watarejea wakiwa imara baaada ya matokeo hayo
Carlinhos anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu, amesema wamepoteza pambano na sio vita, lengo lao la kushinda ubingwa msimu huu bado liko palepale
"Tumepoteza pambano na sio vita, mdhaifu akianguka hainuki lakini bingwa akianguka lazima aamke tena. Mwaka huu Tanzania itakuwa ya njano na kijani," aliandika Carlinhos kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Baada ya kupoteza mchezo jijini Tanga, Yanga inelekea mkoani Arusha ambako March 07 itacheza na Polisi Tanzania mchezo utakaopigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid
ADVERTISE HERE