Kikosi cha Yanga msimu huu kimedhihirisha kuwa bora zaidi kinapocheza ugenini kuliko hata wanapocheza kunako uwanja wa Benjamin Mkapa
Katika michezo 14 ambayo Yanga imeshinda msimu huu, michezo 8 wamepata ushindi wakiwa ugenini huku wakitoka sare michezo mitatu
Tanzania Prisons, Gwambina na Mbeya City ndizo timu pekee zilizofanikiwa kuambulia alama moja dhidi ya Yanga mkoani
Wananchi wamepania kuendeleza rekodi hii dhidi ya Coastal Union pale uwanja wa Mkwakwani jioni ya leo
Washambuliaji Michael Sarpong, Yacouba Songne na Fiston Abdul Razak leo watakuwa na kazi moja tu, kutumia vyema nafasi
Katika mabao manne aliyofunga, Yacouba amefunga mabao yake matatu nje ya jiji la Dar es salaam
Bila shaka leo kama kocha Cedric Kaze atampa nafasi, anaweza kuendeleza pale alipoishia mwaka 2020